Yohana 7:45-52
Yohana 7:45-52 NENO
Hatimaye wale walinzi wa Hekalu wakarudi kwa viongozi wa makuhani na Mafarisayo waliokuwa wamewatuma ili kumkamata Yesu, wakaulizwa, “Mbona hamkumkamata?” Wale walinzi wakajibu, “Kamwe hajanena mtu yeyote kama yeye anenavyo.” Mafarisayo wakajibu, “Je, nanyi pia mmedanganyika? Je, kuna kiongozi yeyote au mmoja wa Mafarisayo ambaye amemwamini? Lakini umati huu wa watu wasiojua Sheria ya Musa, wamelaaniwa.” Ndipo Nikodemo, yule aliyekuwa amemwendea Yesu siku moja usiku, na alikuwa mmoja wao, akauliza, “Je, sheria zetu zinaturuhusu kumhukumu mtu kabla ya kumsikiliza na kufahamu alilotenda?” Wakamjibu, “Je, wewe pia unatoka Galilaya? Chunguza nawe utaona kwamba hakuna nabii atokae Galilaya!” [