Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yohana 5:10-15

Yohana 5:10-15 NEN

Kwa hiyo Wayahudi wakamwambia yule mtu aliyeponywa, “Leo ni Sabato, si halali wewe kubeba mkeka wako.” Yeye akawajibu, “Yule mtu aliyeniponya aliniambia, ‘Chukua mkeka wako na uende.’  ” Wakamuuliza, “Ni mtu gani huyo aliyekuambia uchukue mkeka wako uende?” Basi yule mtu aliyeponywa hakufahamu ni nani aliyemponya, kwa sababu Yesu alikuwa amejiondoa katika ule umati wa watu uliokuwa hapo. Baadaye Yesu akamkuta yule mtu aliyemponya ndani ya Hekalu na kumwambia, “Tazama umeponywa, usitende dhambi tena. La sivyo, lisije likakupata jambo baya zaidi.” Yule mtu akaenda, akawaambia wale Wayahudi kuwa ni Yesu aliyemponya.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Yohana 5:10-15

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha