Yohana 13:21-25
Yohana 13:21-25 NENO
Baada ya kusema haya, Yesu alifadhaika sana moyoni, akasema, “Amin, amin nawaambia, mmoja wenu atanisaliti.” Wanafunzi wake wakatazamana bila kujua kuwa alikuwa anamsema nani. Mmoja wa wanafunzi wake, ambaye Yesu alimpenda sana, alikuwa ameegama kifuani mwa Yesu. Simoni Petro akampungia mkono yule mwanafunzi, akamwambia, “Muulize anamaanisha nani.” Yule mwanafunzi akamwegemea Yesu, akamuuliza, “Bwana, tuambie, ni nani?”