Yeremia 51:15-16
Yeremia 51:15-16 NENO
“Aliiumba dunia kwa uweza wake; akaweka misingi ya ulimwengu kwa hekima yake, na akazitandaza mbingu kwa ufahamu wake. Atoapo sauti yake, maji yaliyo katika mbingu hunguruma; huyafanya mawingu yainuke kutoka miisho ya dunia. Hupeleka miali ya radi pamoja na mvua, naye huuleta upepo kutoka ghala zake.

