Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yeremia 1:9-14

Yeremia 1:9-14 NENO

Kisha BWANA akaunyoosha mkono wake na kugusa kinywa changu, akaniambia, “Sasa nimeyaweka maneno yangu kinywani mwako. Tazama, leo nimekuweka juu ya mataifa na falme ili kungʼoa na kubomoa, kuharibu na kuangamiza, kujenga na kupanda.” Neno la BWANA likanijia kusema, “Je, Yeremia unaona nini?” Nami nikajibu, “Naona tawi la mti wa mlozi.” BWANA akaniambia, “Umeona vyema kwa maana ninaliangalia neno langu ili kuona kwamba limetimizwa.” Neno la BWANA likanijia tena, “Unaona nini?” Nikajibu, “Naona chungu kinachochemka, kikiwa kimeinama kutoka kaskazini.” BWANA akaniambia, “Kutoka kaskazini maafa yatamwagwa kwa wote wanaoishi katika nchi.