Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 5:1-7

Isaya 5:1-7 NENO

Nitaimba wimbo kwa mpenzi wangu, wimbo kuhusu shamba lake la mizabibu: Mpenzi wangu alikuwa na shamba la mizabibu kwenye kilima chenye rutuba. Alililima na kuondoa mawe na akaliotesha mizabibu bora sana. Akajenga mnara wa ulinzi ndani yake, na kutengeneza shinikizo la kukamulia zabibu pia. Kisha akatazamia kupata mazao ya zabibu nzuri, lakini lilizaa matunda mabaya tu. “Basi enyi wakazi wa Yerusalemu na watu wa Yuda, hukumuni kati yangu na shamba langu la mizabibu. Ni nini zaidi ambacho kingefanyika katika shamba langu la mizabibu kuliko yale niliyofanya? Nilipotazamia kupata zabibu nzuri, kwa nini lilizaa zabibu mbaya tu? Sasa nitawaambia lile nitakalolitendea shamba langu la mizabibu: Nitaondoa uzio wake, nalo litaharibiwa, nitabomoa ukuta wake, nalo litakanyagwa. Nitalifanya nchi ya ukiwa isiyokaliwa na watu, halitakatiwa matawi wala kulimwa, nayo michongoma na miiba itamea huko, nitaamuru mawingu yasinyeshe mvua juu yake.” Shamba la mzabibu la BWANA wa majeshi ni nyumba ya Israeli, na watu wa Yuda ni bustani yake ya kumpendeza. Alitazamia haki, lakini akaona umwagaji damu; alitazamia uadilifu, lakini akasikia vilio vya taabu.