Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 7:17-24

Mwanzo 7:17-24 NENO

Kwa siku arobaini mafuriko yaliendelea kujaa duniani; maji yalivyozidi kuongezeka, yaliinua safina juu sana kutoka uso wa dunia. Maji yakajaa na kuongezeka sana juu ya dunia, na safina ikaelea juu ya maji. Maji yakazidi kujaa juu ya dunia, yakaifunika milima yote mirefu chini ya mbingu yote. Maji yakaendelea kujaa, yakaifunika milima kwa kina cha zaidi ya dhiraa kumi na tano. Kila kiumbe hai kinachotambaa juu ya dunia kikaangamia: ndege, mifugo, wanyama pori, viumbe vyote juu ya nchi, na wanadamu wote. Kila kiumbe juu ya nchi kavu chenye pumzi ya uhai kikafa. Kila kitu chenye uhai juu ya uso wa nchi kilifutiliwa mbali; watu, wanyama pori, viumbe vinavyotambaa ardhini, na ndege warukao angani wakafutiliwa mbali toka duniani. Waliobaki ni Nuhu peke yake na wale waliokuwa pamoja naye ndani ya safina. Maji yakaifunika dunia kwa siku mia moja na hamsini.