Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ezekieli Utangulizi

Utangulizi
Kitabu hiki kimepewa jina la nabii Ezekieli ambaye maana yake ni “Mungu ni Mwenye Nguvu.” Alizaliwa katika jamii ya kikuhani na kulelewa katika mazingira ya hekalu huko Yerusalemu. Mnamo mwaka wa 597 K.K. Ezekieli alikuwa mmoja wa mateka 10,000 waliopelekwa uhamishoni Babeli. Mungu alimwita katika huduma mwaka wa 593 K.K. kwa njia ya ufunuo.
Katika sehemu ya kwanza ya huduma yake alitoa ujumbe ule ule ambao Yeremia aliutangaza kwamba mji wa Yerusalemu na Hekalu vingeliharibiwa. Wingi wa dhambi na kuabudu sanamu kulikokuwa kunaendelea huko Yerusalemu kungelisababisha Mungu kuliacha Hekalu na Yerusalemu pia, kukifuatiwa na hukumu. Kuja kwa Babeli kuteka na kuharibu kulikuwa ni uhakikisho.
Baada ya habari kufika Babeli mwaka wa 586 K.K. kwamba Yerusalemu ilikuwa imeangamizwa, Ezekieli alitangaza ujumbe mpya wa matumaini ya kurudishwa kwa Waisraeli. Kama Mchungaji Mkuu, Mungu angewakusanya tena Waisraeli kutoka miisho ya dunia na kuwaimarisha tena katika nchi yao wenyewe. Mataifa ambayo yangeleta upinzani kuhusu kurudi kwa Waisraeli wangeshindwa na kuhukumiwa.
Mwandishi
Ezekieli mwana wa Buzi.
Kusudi
Kutangaza hukumu ya Mungu dhidi ya Wayahudi na mataifa mengine, na kuelezea wokovu wa watu wa Mungu.
Mahali
Babeli.
Tarehe
Kama mwaka wa 571 K.K.
Wahusika Wakuu
Ezekieli, viongozi wa Israeli, mke wa Ezekieli, Nebukadneza.
Wazo Kuu
Kuwaonya watu juu ya dhambi zao na kutokutii. Kuonyesha pia wema wa Mungu kwa watu wake na kuweka wazi rehema za Mungu endapo watu wangetubu.
Mambo Muhimu
Ujumbe wa Mungu kwa taifa la Israeli kuhusu hukumu ya dhambi zao, hukumu ya watu wa mataifa, na tumaini kwa watu wa Israeli kwa siku za mwisho.
Mgawanyo
Mwito wa Ezekieli (1:1–3:27)
Hali ya dhambi ya Yerusalemu na maangamizi (4:1–24:27)
Unabii dhidi ya mataifa ya kigeni (25:1–32:32)
Matumaini ya kurudishwa upya (33:1–39:29)
Israeli kurudishwa kwenye nchi yao (40:1–48:35).

Iliyochaguliwa sasa

Ezekieli Utangulizi: NEN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha