Waefeso Utangulizi
Utangulizi
Paulo aliandika waraka huu akiwa gerezani huko Rumi ili kuwatia moyo waumini wa jimbo la Asia. Waraka huu ulikuwa kama mwongozo uliokusudiwa kwa makanisa kadhaa. Zaidi ya hayo, kwenye waraka huu hakuna salamu za watu binafsi, wala hakuna matatizo maalum. Paulo alielezea kwamba kanisa lilianzishwa na Mungu, akiwaelezea mpango wa Mungu wa tangu awali wa kuwaokoa watu wake kupitia Kristo kwa imani. Mpango huu ulikuwako hata kabla ya ulimwengu kuumbwa. Mwenendo wa maisha mapya upo kinyume kabisa na ule wa maisha ya kale bila Kristo.
Mwandishi
Mtume Paulo.
Kusudi
Kuwaimarisha waumini katika imani yao ya Kikristo kwa kueleza asili na kusudi la kanisa, ambalo ni mwili wa Kristo.
Mahali
Rumi.
Tarehe
Mnamo 60 B.K.
Wahusika Wakuu
Paulo, Tikiko, na waumini wa Efeso.
Wazo Kuu
Mpango wa Mungu wa milele wa kuuokoa ulimwengu ulitimizwa kupitia kwa Kristo katika mwili wake.
Mambo Muhimu
Umoja katika Kristo na maisha mapya katika Kristo (2:4‑6), na umoja katika mwili wa Kristo. Pia maisha Wakristo wanayopaswa kuishi kuhusu ndoa, tabia, mwenendo, wazazi na watoto, watumishi na mabwana zao.
Yaliyomo
Mpango wa Mungu, na wokovu wa wote wanaomwamini (1:1–2:22)
Siri ya Injili (3:1‑21)
Maisha ya Mkristo duniani (4:1–6:9)
Silaha za Mungu, salamu za mwisho (6:10‑24).
Iliyochaguliwa sasa
Waefeso Utangulizi: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Biblia Takatifu™ Neno™
Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Version™
Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.