Danieli 4:34
Danieli 4:34 NEN
Mwisho wa wakati huo, mimi Nebukadneza niliinua macho yangu kuelekea mbinguni, nazo fahamu zangu zikanirudia. Ndipo nikamsifu Yeye Aliye Juu Sana, nikamheshimu na kumhimidi yeye aishiye milele. Utawala wake ni utawala wa milele; ufalme wake hudumu kizazi hadi kizazi.


