Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Matendo 6:1-4

Matendo 6:1-4 NENO

Basi ikawa katika siku hizo, wakati idadi ya wanafunzi ilipokuwa ikiongezeka sana, Wayahudi wa Kiyunani walinungʼunika dhidi ya Waebrania kwa sababu wajane wao walisahaulika katika mgawo wa chakula wa kila siku. Wale mitume kumi na wawili wakakusanya wanafunzi wote pamoja wakasema, “Haitakuwa vyema sisi kuacha huduma ya neno la Mungu ili kuhudumu mezani. Kwa hiyo ndugu, chagueni watu saba miongoni mwenu, watu wenye sifa njema, waliojawa na Roho Mtakatifu na hekima, ambao tunaweza kuwakabidhi kazi hii, nasi tutatumia muda wetu kuomba na katika huduma ya neno.”