Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Matendo 24:10-21

Matendo 24:10-21 NENO

Mtawala Feliksi alipompungia Paulo mkono ili ajitetee, yeye akajibu, “Najua kwamba wewe umekuwa hakimu katika taifa hili kwa miaka mingi, hivyo natoa utetezi wangu kwa furaha. Unaweza kuhakikisha kwa urahisi kuwa hazijapita zaidi ya siku kumi na mbili tangu nilipopanda kwenda Yerusalemu kuabudu. Hawa wanaonishtaki hawakunikuta nikibishana na mtu yeyote Hekaluni au kuchochea umati wa watu katika sinagogi au mahali pengine popote mjini. Wala hawawezi kabisa kukuthibitishia mashtaka haya wanayoleta dhidi yangu. Lakini ninakubali kwamba mimi namwabudu Mungu wa baba zetu kama mfuasi wa Njia Ile, ambayo wao wanaiita dhehebu. Ninaamini kila kitu kinachokubaliana na Sheria na kile kilichoandikwa katika Manabii, nami ninalo tumaini kwa Mungu, ambalo hata wao wenyewe wanalikubali kwamba kutakuwa na ufufuo wa wafu, kwa wenye haki na wasio na haki. Kwa hiyo ninajitahidi siku zote kuwa na dhamiri safi mbele za Mungu na mbele za wanadamu. “Basi, baada ya miaka mingi nilikuja Yerusalemu ili kuwaletea watu wangu msaada kwa ajili ya maskini na kutoa dhabihu. Nilikuwa nimetakaswa waliponikuta Hekaluni nikifanya mambo haya. Hapakuwa na umati wa watu pamoja nami, wala sikuhusika katika ghasia yoyote. Lakini kuna Wayahudi fulani kutoka jimbo la Asia ambao walipaswa kuwa hapa mbele yako na kunishtaki kama wana jambo lolote dhidi yangu. Au, watu hawa walio hapa waseme ni kosa gani walilonipata nalo waliponisimamisha mbele ya Baraza la Wayahudi, isipokuwa ni kuhusu jambo hili moja nililopaza sauti mbele yao na kusema, ‘Mimi nashtakiwa mbele yenu leo kwa sababu ya ufufuo wa wafu.’ ”

Video ya Matendo 24:10-21