3 Yohana Utangulizi
Utangulizi
Waraka wa tatu wa Yohana uliandikiwa Gayo, ambaye alikuwa kiongozi muhimu katika kanisa. Alielekezwa kuwasaidia na kuwahudumia wajumbe wa Mungu waliotembea kanisani. Pia alipewa onyo kuhusu Deotrefe, kwa tabia yake ya kukosa ushirikiano. Yohana alieleza tarajio lake la kuja na kushughulikia tatizo hili mwenyewe.
Mwandishi
Mtume Yohana.
Kusudi
Yohana anamwandikia Gayo akimpa onyo kuhusu Deotrefe, kwa tabia yake ya kukosa ushirikiano.
Mahali
Efeso.
Tarehe
Mnamo 90 B.K.
Wahusika Wakuu
Yohana, Gayo, Deotrefe, na Demetrio.
Wazo Kuu
Wajibu binafsi wa Gayo kuhusu watumishi wa kweli na wa uongo.
Mambo Muhimu
Yohana anamtakia Gayo kufanikiwa katika mambo yote, na pia anamwagiza asiige lililo baya bali aige lililo jema.
Yaliyomo
Salamu (1‑4)
Gayo anatiwa moyo (5‑8)
Deotrefe anakemewa (9‑10)
Demetrio anasifiwa (11‑12)
Hitimisho (13‑15).
Iliyochaguliwa sasa
3 Yohana Utangulizi: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Biblia Takatifu™ Neno™
Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Version™
Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.