Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Wakorintho 2:5-11

2 Wakorintho 2:5-11 NEN

Lakini ikiwa mtu yeyote amesababisha huzuni, kwa kiasi fulani hakunihuzunisha mimi kama vile alivyowahuzunisha ninyi nyote, ili nisiwe mkali kupita kiasi. Adhabu hii aliyopewa na wengi inamtosha. Basi sasa badala yake, inawapasa kumsamehe na kumfariji, ili asigubikwe na huzuni kupita kiasi. Kwa hiyo, nawasihi, mpate kuuthibitisha tena upendo wenu kwa ajili yake. Sababu ya kuwaandikia ni kuona kama mngeweza kushinda hilo jaribio na kutii katika kila jambo. Kama ninyi mkimsamehe mtu yeyote, mimi pia nimemsamehe. Kile nilichosamehe, kama kulikuwa na kitu chochote cha kusamehe, nimekwisha kusamehe mbele ya Kristo kwa ajili yenu, ili Shetani asitushinde. Kwa maana hatuachi kuzijua hila zake.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na 2 Wakorintho 2:5-11

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha