Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Nyakati Utangulizi

Utangulizi
Kitabu cha 2 Mambo ya Nyakati kinaendelea kuelezea historia ya Yuda. Sura za 1–9 zinaelezea kujengwa kwa Hekalu wakati wa utawala wa Mfalme Sulemani. Sura za 10–36 zinaelezea historia ya Ufalme wa Yuda hadi kufikia kuharibiwa kwa Yerusalemu na watu kupelekwa uhamishoni Babeli. Kitabu hiki kinazungumzia jinsi uhusiano wa watu na Mungu ni jambo la muhimu kuliko vitu vyote. Kitabu cha 2 Mambo ya Nyakati kinaambatana na vitabu vya 1 na 2 Wafalme, kikitoa ufafanuzi wake. Ufalme wa Kaskazini, yaani Israeli, haujatajwa kabisa katika historia ya kitabu hiki.
Mwandishi
Mapokeo ya Kiyahudi husema ni Ezra.
Kusudi
Kuliunganisha taifa katika ibada ya Mungu wa kweli kwa kuonesha viwango vyake katika kuwahukumu wafalme. Habari za wafalme wenye haki wa Yuda, dhambi za wafalme waovu, na wapinzani wao wa kidini nyakati za utawala wao zimewekwa wazi.
Mahali
Yerusalemu, na katika Hekalu.
Tarehe
Kama mwaka wa 430 K.K.
Wahusika Wakuu
Sulemani, Malkia wa Sheba, Rehoboamu, Asa, Yehoshafati, Yehoramu, Yoashi, Uzia, Ahazi, Hezekia, Manase na Yosia.
Wazo Kuu
Kitabu hiki kinaonesha mpango wa Mungu kwa Israeli. Pia kinaonesha kwa nini ufalme wa Daudi haukuruhusiwa kuendelea kwa muda mrefu. Kitabu hiki, kama kile cha kwanza, kinaonesha wajibu wa Mungu katika historia ya watu wake na mwingiliano kati ya maisha ya kiroho na ya kisiasa. Wafalme wanapimwa kwa jinsi walivyokuwa waaminifu kwa Mungu.
Mambo Muhimu
Utawala wa Sulemani, kujengwa kwa Hekalu, kuasi kwa makabila kumi, habari za wafalme wa Yuda, na kuharibiwa kwa ufalme wa Yuda na Wababeli mwaka wa 586 K.K.
Yaliyomo
Utawala wa Sulemani (1:1–9:31)
Wafalme wa Yuda (10:1–36:14)
Kuanguka kwa Yerusalemu (36:15‑23).

Iliyochaguliwa sasa

2 Nyakati Utangulizi: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia