BWANA akasema na Manase pamoja na watu wake, lakini hawakumjali. Hivyo BWANA akaleta juu yao majemadari wa jeshi la mfalme wa Ashuru, ambao walimchukua Manase kwenda kifungoni, wakaweka ndoana katika pua yake, wakamfunga kwa pingu za shaba na kumpeleka Babeli. Katika dhiki yake akamsihi BWANA Mungu wake na kujinyenyekeza sana mbele za Mungu wa baba zake. Naye alipomwomba, BWANA akaguswa na kule kusihi kwake na akasikiliza kilio chake, kwa hiyo akamrudisha Yerusalemu na kwenye ufalme wake. Ndipo Manase akatambua kwamba BWANA ndiye Mungu.
Soma 2 Nyakati 33
Sikiliza 2 Nyakati 33
Shirikisha
linganisha matoleo yote: 2 Nyakati 33:10-13
Hifadhi mistari, soma bila mtandao, tazama klipu za mafunzo, na zaidi!
YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video