Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Wathesalonike 5:1-8

1 Wathesalonike 5:1-8 NENO

Basi ndugu, hatuna haja ya kuwaandikia kuhusu nyakati na majira, kwa kuwa mnajua vyema kwamba siku ya Bwana itakuja kama mwizi anavyokuja usiku. Watu wanaposema, “Kuna amani na salama,” maangamizi huwajia ghafula, kama vile uchungu unavyomjia mwanamke mwenye mimba; nao hakika hawatatoroka. Bali ninyi, ndugu, hampo gizani hata siku ile iwakute ghafula kama mwizi. Ninyi nyote ni wana wa nuru na wana wa mchana. Sisi si wana wa giza wala wa usiku. Kwa hiyo basi, tusilale kama watu wengine wanavyolala, bali tukeshe na kuwa na kiasi. Kwa kuwa wote wanaolala, hulala usiku, na wale wanaolewa, hulewa usiku. Lakini kwa kuwa sisi ni wana wa mchana, basi tuwe na kiasi, tukijivika imani na upendo kama dirii kifuani na tumaini letu la wokovu kama chapeo.