1 Petro Utangulizi
Utangulizi
Mtume Petro ni mmoja wa wale wanafunzi kumi na wawili wa Yesu. Aliandikia waraka huu kwa Wakristo wa Kiyahudi waliotawanyika huko sehemu ya Asia Ndogo. Waraka huu unaonesha kwamba waumini walikuwa wanakabiliwa na dhiki na mateso. Lengo lake lilikuwa kuwafariji waumini walioishi jimbo la Asia, kwani katika kipindi hiki cha miaka ya sitini ya karne ya kwanza, utawala wa Rumi chini ya Nero ulianza kuwatesa Wakristo.
Kwa wale waliokuwa wakifikiria kurudia imani yao ya Kiyahudi ili kuepuka mateso, anawaambia kuwa sasa kanisa ndilo ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu walio milki yake Mungu. Hivyo mawazo ya kurejea imani ya Kiyahudi hayana faida yoyote. Kisha Petro anatoa mfano wa Kristo na jinsi alivyopata mateso, na anawakumbusha waumini kuwa wao pia hawana budi kupata mateso. Mwishowe, Petro anatoa maagizo kwa vikundi mbalimbali vya Wakristo.
Mwandishi
Mtume Petro.
Kusudi
Kuwatia moyo Wakristo kusimama dhabiti katika mateso yote, na kuwa imara katika neema ya Mungu.
Mahali
Rumi.
Tarehe
Mnamo 63 B.K.
Wahusika Wakuu
Petro, Silvano, na Marko.
Wazo Kuu
Hata kama tutauawa kwa ajili ya imani, tushikilie imani yetu. Mungu anafahamu yote yanayotendeka, na katika mpango wake wa milele, hatimaye mambo yote yatakamilika kwa utukufu wake.
Mambo Muhimu
Petro anaonesha kwamba mateso ni sehemu ya maisha ya Kikristo, na kwamba Mungu ameandaa thawabu zisizoharibika kwa wote wanaomwamini. Pia anaonesha tumaini la wakati wa mwisho kuwa jambo la kumtia moyo muumini katika mateso.
Yaliyomo
Salamu, utukufu wa wokovu wa Kristo (1:1‑25)
Utiifu wa Mkristo (2:1‑25)
Maisha yampasayo Mkristo (3:1–4:11)
Huduma ya Kikristo, na salamu za mwisho (4:12–5:14).
Iliyochaguliwa sasa
1 Petro Utangulizi: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Biblia Takatifu™ Neno™
Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Version™
Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.