Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Nyakati 26

26
Mabawabu
1Hii ndiyo migawanyo ya mabawabu:
Kutoka kwa wana wa Kora alikuwa:
Meshelemia mwana wa Kore, mmoja wa wana wa Asafu. 2Meshelemia alikuwa na wana wafuatao:
Zekaria mzaliwa wa kwanza, Yediaeli wa pili,
Zebadia wa tatu, Yathnieli wa nne,
3Elamu wa tano, Yehohanani wa sita,
na Eliehoenai wa saba.
4Obed-Edomu naye alikuwa na wana wafuatao:
Shemaya mzaliwa wa kwanza, Yehozabadi wa pili,
Yoa wa tatu, Sakari wa nne,
Nethaneli wa tano, 5Amieli wa sita,
Isakari wa saba, na Peulethai wa nane.
(Kwa kuwa Mungu alikuwa amembariki Obed-Edomu.)
6Shemaya mwanawe Obed-Edomu pia alikuwa na wana waliokuwa viongozi katika jamaa ya baba yao, kwa sababu walikuwa watu wenye uwezo mkubwa. 7Wana wa Shemaya ni:
Othni, Refaeli, Obedi na Elizabadi;
jamaa zake Elihu na Semakia walikuwa pia watu wenye uwezo.
8Hawa wote walikuwa wazao wa Obed-Edomu; wao na wana wao na jamaa zao walikuwa watu wenye uwezo na nguvu za kufanya kazi. Wazao wa Obed-Edomu jumla yao walikuwa sitini na wawili.
9Meshelemia alikuwa na wana na jamaa zake, waliokuwa watu wenye uwezo: jumla yao watu kumi na wanane.
10Hosa, Mmerari, alikuwa na wana wafuatao:
Shimri alikuwa mkuu wao (baba yake alikuwa amemweka yeye kuwa mkuu, ijapokuwa hakuwa mzaliwa wa kwanza),
11Hilkia wa pili, Tabalia wa tatu
na Zekaria wa nne.
Wana na jamaa za Hosa jumla yao walikuwa watu kumi na watatu.
12Hii migawanyo ya mabawabu, kupitia wakuu wao, walikuwa na zamu za kuhudumu hekaluni mwa Bwana kama jamaa zao walivyokuwa nazo. 13Kura zilipigwa kwa kila lango, kufuatana na jamaa zao, wakubwa kwa wadogo.
14Kura ya Lango la Mashariki ilimwangukia Shelemia#26:14 au Meshelemia.
Kisha wakapiga kura kwa Zekaria mwanawe Shelemia, aliyekuwa mshauri mwenye hekima, nayo kura ya Lango la Kaskazini ikamwangukia.
15Kura ya Lango la Kusini ikamwangukia Obed-Edomu, nayo kura ya maghala ikawaangukia wanawe.
16Kura za Lango la Magharibi na Lango la Shalekethi kwenye barabara ya juu zikawaangukia Shupimu na Hosa.
Zamu za walinzi ziligawanywa kwa usawa:
17Kulikuwa na Walawi sita kila siku upande wa mashariki,
wanne upande wa kaskazini,
wanne upande wa kusini,
na wawili wawili kwa mara moja kwenye ghala.
18Kuhusu ukumbi kuelekea magharibi, kulikuwa na wanne barabarani na wawili kwenye ukumbi wenyewe.
19Hii ilikuwa migawanyo ya mabawabu waliokuwa wazao wa Kora na wa Merari.
Watunza hazina na maafisa wengine
20Katika Walawi, Ahiya alikuwa mwangalizi wa hazina za nyumba ya Mungu na mwangalizi wa hazina za vitu vilivyowekwa wakfu.
21Wazao wa Ladani, waliokuwa Wagershoni kupitia Ladani na waliokuwa viongozi wa jamaa za Ladani Mgershoni, walikuwa Yehieli, 22wana wa Yehieli, wana wa Zethamu na wa nduguye Yoeli. Wao walikuwa waangalizi wa hazina za Hekalu la Bwana.
23Kutoka kwa Waamrami, Waishari, Wahebroni na Wauzieli:
24Shebueli, mzao wa Gershomu mwana wa Musa, alikuwa afisa mwangalizi wa hazina. 25Jamaa zake kutoka kwa Eliezeri, wanawe walikuwa: Rehabia, Yeshaya, Yoramu, Zikri na Shelomithi.
26Shelomithi na jamaa zake walikuwa waangalizi wa hazina zote za vitu vile vilivyowekwa wakfu na Mfalme Daudi, kwa viongozi wa jamaa waliokuwa majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, na kwa maafisa wengine wa jeshi. 27Baadhi ya nyara zilizotekwa vitani waliziweka wakfu kwa ajili ya ukarabati wa Hekalu la Bwana. 28Kila kitu kilichokuwa kimewekwa wakfu na Samweli mwonaji, na Sauli mwana wa Kishi, Abneri mwana wa Neri, na Yoabu mwana wa Seruya, pamoja na vitu vingine vyote vilivyokuwa vimewekwa wakfu, vyote vilikuwa chini ya uangalizi wa Shelomithi na jamaa zake.
29Kutoka kwa wana wa Ishari:
Kenania na wanawe walipewa kazi nje ya Hekalu kama maafisa na waamuzi juu ya Israeli.
30Kutoka kwa wana wa Hebroni:
Hashabia na jamaa zake, watu elfu moja na mia saba wenye uwezo, waliwajibika katika Israeli magharibi mwa Yordani kwa ajili ya kazi zote za Bwana na utumishi wa mfalme. 31Kuhusu wana wa Hebroni, Yeria alikuwa mkuu wao kufuatana na orodha ya jamaa yao.
Katika mwaka wa arobaini wa utawala wa Daudi, uchunguzi ulifanyika katika kumbukumbu, nao watu wenye uwezo miongoni mwa wana wa Hebroni wakapatikana huko Yazeri katika Gileadi. 32Yeria alikuwa na jamaa ya watu elfu mbili mia saba waliokuwa watu wenye uwezo na viongozi wa jamaa, naye Mfalme Daudi akawaweka kuangalia Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila Manase kuhusu kila jambo lililomhusu Mungu na shughuli za mfalme.

Iliyochaguliwa sasa

1 Nyakati 26: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia