Wakakusanyika pamoja na wazee, wakala njama, wakatoa fedha nyingi za kuwapa wale askari, wakawaambia: Semeni: Wanafunzi wake wamekuja usiku, wakamwiba, sisi tulipokuwa tumelala! Neno hili likijulikana kwa mtawala nchi, sisi tutasema naye kwa werevu, ninyi msipate mahangaiko. Kwa hiyo wakazichukua zile fedha, wakafanya kama walivyofundishwa. Nalo neno hili linasimuliwa kwa Wayuda mpaka leo.