Ndivyo, asemavyo Bwana: Sasa Zerubabeli, jipe moyo! Nawe mtambikaji mkuu Yosua, mwana wa Yosadaki, jipe moyo! Nanyi nyote mlio ukoo wa nchi hii, jipeni mioyo! Ndivyo, asemavyo Bwana: Fanyeni kazi, kwani mimi niko pamoja nanyi! ndivyo, asemavyo Bwana Mwenye vikosi.