1
Hesabu 21:8
Neno
NEN
BWANA akamwambia Musa, “Tengeneza nyoka wa shaba na umweke juu ya mti; yeyote aliyeumwa na nyoka anaweza kumtazama na akaishi tena.”
Linganisha
Chunguza Hesabu 21:8
2
Hesabu 21:9
Kwa hiyo Musa akatengeneza nyoka wa shaba na kumweka juu ya mti. Kisha wakati mtu yeyote aliumwa na nyoka, naye akamtazama yule nyoka wa shaba, aliishi.
Chunguza Hesabu 21:9
3
Hesabu 21:5
wakamnungʼunikia Mungu na Musa, wakisema, “Kwa nini umetupandisha kutoka Misri ili tufe jangwani? Hakuna mkate! Hakuna maji! Nasi tunachukia sana chakula hiki duni!”
Chunguza Hesabu 21:5
4
Hesabu 21:6
Ndipo BWANA akapeleka nyoka wenye sumu kati yao; wakawauma watu, nao Waisraeli wengi wakafa.
Chunguza Hesabu 21:6
5
Hesabu 21:7
Watu wakamjia Musa na kusema, “Tumetenda dhambi wakati tuliponena dhidi ya BWANA na dhidi yako. Mwombe BWANA ili atuondolee hawa nyoka.” Hivyo Musa akawaombea hao watu.
Chunguza Hesabu 21:7