1
Yoshua 10:13
Neno: Bibilia Takatifu 2025
NENO
Hivyo jua likasimama, nao mwezi ukatulia, hadi taifa hilo lilipokwisha kujilipizia kisasi kwa adui zake, kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Yashari. Jua likasimama katikati ya mbingu, likachelewa kuzama muda wa siku nzima.
Linganisha
Chunguza Yoshua 10:13
2
Yoshua 10:12
Siku ile BWANA alipowakabidhi Waamori kwa Waisraeli, Yoshua akanena na BWANA akiwa mbele ya Waisraeli, akasema: “Wewe jua, simama juu ya Gibeoni, wewe mwezi, tulia juu ya Bonde la Aiyaloni.”
Chunguza Yoshua 10:12
3
Yoshua 10:14
Hakujakuwa na siku nyingine kama hiyo kabla au baada, siku ambayo BWANA alimsikiliza mwanadamu. Hakika BWANA alikuwa akiwapigania Israeli.
Chunguza Yoshua 10:14
4
Yoshua 10:8
BWANA akamwambia Yoshua, “Usiwaogope watu hao, nimewatia mkononi mwako. Hakuna yeyote atakayeweza kushindana nawe.”
Chunguza Yoshua 10:8
5
Yoshua 10:25
Yoshua akawaambia, “Msiogope, wala msivunjike moyo. Kuweni hodari na wenye ushujaa. Hili ndilo BWANA atakalowatendea adui zenu wote mnaoenda kupigana nao.”
Chunguza Yoshua 10:25
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video