Ndipo Daudi akamwambia Abishai na maafisa wake wote, “Mwanangu, ambaye ametoka viunoni mwangu mwenyewe, anajaribu kuniua. Je, si zaidi sana huyu Mbenyamini! Mwacheni; acha alaani, kwa maana BWANA amemwambia afanye hivyo. Inawezekana kwamba BWANA ataona dhiki yangu na kunilipa mema kwa ajili ya laana ninayopokea leo.”