1
1 Wathesalonike 5:16-18
Neno: Bibilia Takatifu 2025
NENO
Furahini siku zote; ombeni bila kukoma; shukuruni kwa kila jambo, kwa maana haya ndio mapenzi ya Mungu kwa ajili yenu katika Kristo Yesu.
Linganisha
Chunguza 1 Wathesalonike 5:16-18
2
1 Wathesalonike 5:23-24
Mungu mwenyewe, Mungu wa amani, awatakase ninyi kabisa. Nanyi mhifadhiwe roho zenu, nafsi zenu na miili yenu, bila kuwa na lawama katika Bwana wetu Yesu Kristo. Yeye aliyewaita ni mwaminifu naye atafanya hayo.
Chunguza 1 Wathesalonike 5:23-24
3
1 Wathesalonike 5:15
Angalieni kuwa mtu asimlipe mwenzake maovu kwa maovu, bali siku zote tafuteni kutendeana mema ninyi kwa ninyi na kwa watu wote.
Chunguza 1 Wathesalonike 5:15
4
1 Wathesalonike 5:11
Kwa hiyo farijianeni na kujengana, kama vile mnavyofanya sasa.
Chunguza 1 Wathesalonike 5:11
5
1 Wathesalonike 5:14
Nasi twawasihi, ndugu, waonyeni walio wavivu, watieni moyo waoga, wasaidieni wanyonge na kuwavumilia watu wote.
Chunguza 1 Wathesalonike 5:14
6
1 Wathesalonike 5:9
Kwa maana Mungu hakutuita ili tupate ghadhabu bali tupate wokovu kupitia kwa Bwana wetu Yesu Kristo.
Chunguza 1 Wathesalonike 5:9
7
1 Wathesalonike 5:5
Ninyi nyote ni wana wa nuru na wana wa mchana. Sisi si wana wa giza wala wa usiku.
Chunguza 1 Wathesalonike 5:5
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video