Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Rum 8:6

Kuweka Muda Wa Kupumzika
siku 5
Kupenda kazi sana na wakati wote kufanya kazi vinasifiwa sana katika ulimwengu wetu, na vinaweza kuwa ni changamoto kwa wengine. Ili kutimiza majukumu yetu na mipango yetu kwa ufanisi, lazima tujifunze kupumzika au hatutakuwa na cha kuchangia kwa tunaowapenda na kwa malengo tuliyoyaweka. Hebu tuchukue siku tano zijazo kujifunza kuhusu kupumzika na jinsi tunavyoweza kutumia tuliyojifunza maishani mwetu.

Hatua Sita Ya Uongozi Bora Zaidi
Siku 7
U tayari kukua kama kiongozi? Craig Groeschel anafafanua hatua sita ya kibiblia yeyote anaweza kuchukua ili kuwa kiongozi bora zaidi. Gundua nidhamu ya kuanza, ujasiri wa kuacha, mtu wa kumwezesha, mfumo wa kuumba, uhusiano wa kuanzilisha, na hatari ambayo unahitaji kuchukua.

Mwaka Mpya, Rehema Mpya
SIku 15
Kwa siku 15 zifuatazo, Paul David Tripp atakukumbusha kuhusu neema ya Mungu kwako—ukweli ambao daima si wa kale. Wakati ambapo “urekebishaji wa tabia” na semi za kukutia moyo hazitoshi kukufanya uwe mtu mpya, jifunze kutumainia wema wa Mungu, kutegemea neema yake, na kuishi kwa ajili ya utukufu wake kila siku.