Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Rum 8:16

Uhakika
Siku 4
Mungu anataka UJUE umeokolewa na utaenda mbinguni! Uhakika wako unakua kupitia kukutana na Mungu na kutafakari neno lake. Mistari inayofuata, unapoikariri, inaweza kukusaidia kuwa na uhakika katika Mungu siku zako zote. Maisha yako yabadilishwe kwa kukariri maandiko! Kwa mfumo kamili wa kukariri maandiko, tembelea MemLok.com

Waliochaguliwa: Jikumbushe Kuhusu Injili Kila Siku
Siku 7
Kutatokea nini kama utaamka kila siku na kijikumbusha juu ya injili? Masomo haya ya siku 7 yanalenga kukukumbusha hilo! Injili si kwamba inatuokoa tuu, bali hutuimarisha pia katika maisha yetu yote. Mwandishi na Mwinjilisti Matt Brown ametayarisha mpango huu wa masomo ambayo yanapatikana katika kitabu chake cha masomo ya siku 30 kilichoandikwa na Matt Brown na Ryan Skoog.

Mwaka Mpya, Rehema Mpya
SIku 15
Kwa siku 15 zifuatazo, Paul David Tripp atakukumbusha kuhusu neema ya Mungu kwako—ukweli ambao daima si wa kale. Wakati ambapo “urekebishaji wa tabia” na semi za kukutia moyo hazitoshi kukufanya uwe mtu mpya, jifunze kutumainia wema wa Mungu, kutegemea neema yake, na kuishi kwa ajili ya utukufu wake kila siku.