Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Rum 12:2

Kuishi mabadiliko ya Mungu.
Siku 5
Kua kiumbe kipya ndani ya Kristo inamaanisha kwamba tukonafanyika upya mara kwa mara kumupitia. Mungu hufanya upya roho zetu, akili, na mwili. Anafanya upya pia hata madhumuni yetu. Kati ya siku hizi 5 za mpango wa usomaji, utapiga mbizi zaidi ndani ya Neno ambalo Mungu husema kuhusu kufanyika upya. Kila siku, utapata usomi wa Bibilia na ibada kwa ufupi ambayo itakusaidia kwa njia kadhaa ya kuishi pia kufanyika upya na Mungu.

Kupata Uhuru kutokana na Kufadhaika
Siku 5
Kufadhaika huwa, lakini hakufai kuyaendesha maisha yako. Kumpitia Kristo, tunaweza kuibadilisha, kuiona upya na kuitafsiri upya. Kama unapata changamoto na kufadhaika, angalia mpango huu wa Bibilia wa siku 5 ili ujifunze kupata uhuru na amani.

Kuweka Muda Wa Kupumzika
siku 5
Kupenda kazi sana na wakati wote kufanya kazi vinasifiwa sana katika ulimwengu wetu, na vinaweza kuwa ni changamoto kwa wengine. Ili kutimiza majukumu yetu na mipango yetu kwa ufanisi, lazima tujifunze kupumzika au hatutakuwa na cha kuchangia kwa tunaowapenda na kwa malengo tuliyoyaweka. Hebu tuchukue siku tano zijazo kujifunza kuhusu kupumzika na jinsi tunavyoweza kutumia tuliyojifunza maishani mwetu.

Maombi Ya Kusudi Katika Ndoa Yako
Siku 6
Kamwe katika historia ya ulimwengu taasisi ya ndoa haijawahi kuwa chini ya chunguzi kama ilivyo. Kila siku, jamii hutafuta kufafanua upya maana ya kuoa, na Wakristo wanakabiliwa na ukosoaji mkubwa zaidi kwa kushikilia kile kinachoitwa mtazamo na wa mawazo finyu kuhusu ndoa. Kwa hivyo kusudi la kibiblia la ndoa ni nini, na tunapaswa kuombaje kama waumini ili kuhifadhi maana yake? Katika kampeni yetu ya siku sita, Maombi ya Kusudi katika Ndoa Yako, wanandoa wanaweza kuomba kuwepo na maana katika ndoa yao wenyewe, na pia kuthibitisha ufahamu wa kimungu wa muungano wa agano kati ya mwanamume na mwanamke.

Nenda Tenda Sema Toa: Uhuru wa Kujisalimisha kwa Yesu
Siku 7
Kujisalimisha kwa Yesu ni tukio kubwa maishani. Lakini uamuzi huu unamaanisha nini na tutauishi vipi kila siku? Uamuzi ni wa mambo makubwa ya maisha pekee, ama wacha Mungu kupita kiasi? Woga, makosa yaliyopita, na kutoelewa vinaweza kutuzuia. "Nenda Tenda Sema Toa" ni ahadi/sala ambayo inafunua jinsi utakavyochukua hatua zinazofuata katika safari yako ya kiroho. Pata uhuru unaotokana na kumfuata Yesu.

Maombi Hatari
Siku 7
Umechoka kujali usalama katika imani yako? Uko tayari kukabili hofu zako, kujenga imani yako, na kufikia uwezo wako kamili? Mpango huu wa Biblia wa siku 7 kutoka kwenye kitabu cha Mchungaji Craig Groeschel wa Life.Church, "Dangerous Prayers" yaani Maombi Hatari, unakujasiri uombe bila kujali usalama—kwa sababu kumfuata Yesu haukufaa kuwa salama salmini.

Upendo wa Kweli ni nini?
Siku 12
Kila mtu anataka kujua upendo ni kitu gani. Lakini watu wachache huangalia ni nini Biblia inasema kuhusu upendo. Upendo ni mada moja muhimu ya Maandiko na pia wema muhimu zaidi katika maisha ya Kikristo. Mpango huu kutoka Huduma za Thistlebend unashughulikia maana ya kibiblia ya upendo na jinsi ya kuboresha kumpenda Mungu na kuwapenda wengine.

Kutafuta Amani
Siku 10
Unataka amani zaidi katika maisha yako? Unataka utulivu uwe zaidi ya matamanio yako? Unaweza kupata amani kutoka kwenye chanzo kimoja tuu--Mungu. Jiunge na Dkt. Charles Stanley anapokuonesha njia ya kubadilisha amani ya mawazo yako, akikupa nyenzo za kutatua majuto yaliyopita, kukabiliana na wasiwasi wa sasa, na kutuliza wasiwasi wa mambo yajayo.

Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023
Siku 29
Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka na Warumi. Karibu kujiunga na mpango huu