Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mit 3:6

Kuomba Kulingana Na Majina Yake Yesu: Nyota Ya Asubuhi
Siku 4
Dk. Tony Evans anatoa maombi ya jina la Yesu, nyota ya asubuhi. Sala ya kuabudu, maungamo, shukrani na dua kumhusu Nyota ya asubuhi, Yule anayeangazia njia yetu.

Kushinda Kujiamini na Wasiwasi
4 Siku
Mchezaji virukaji wa Uingereza Cindy Sember anashiriki(anaelesea) jinsi alivyoshinda hali ya kutojiamini na wasiwasi katika mashindano. Cindy huwasaidia wanariadha kugeuza mtazamo wao kutoka kwa woga hadi imani, wakitumaini ahadi za Mungu za nguvu. Mpango huu unatoa njia rahisi, za vitendo za kuchukua nafasi ya wasiwasi na uaminifu. Inakusaidia kupata amani na ujasiri katika michezo na maisha. Ni sehemu ya mfululizo wa mashindano ya kutumia kabla, wakati na baada ya kushindana.

Je, nafsi yako
Siku 5
Yuda Smith huwasaidia wasomaji kuchunguza na kuimarisha nafsi zao kama wanavyokua karibu na Mungu.

MUNGU + MALENGO: Jinsi Ya Kuweka Malengo Kama Mkristo
Siku 5
Ni vyema kuweka malengo kama Mkristo. Unajuaje kama lengo lako ni kutoka kwa Mungu au kwako mwenyewe?. Na malengo ya kikristo yanaonekanaje? Katika siku 5 za mpango huu wa kusoma, utajifunza katika neno na kupata ufasaha na muelekeo juu ya kupanga mipango inayosukumwa na neema!

Kukua katika Upendo
Siku 5
Kinachojalisha kwa kweli ni kumpenda Mungu na kuwapenda wengine, lakini tunawapendaje kwa ufanisi? Ukweli ni kwamba, hatuwezi kuwapenda watu vizuri kwa nguvu zetu wenyewe. Lakini tunapomuangalia Mungu na kunyenyekea, tunaweza kuishi katika nguvu kamili ya upendo wa Mungu. Jifunze zaidi kuhusu kukua katika upendo katika mpango wa siku 5 kutoka wa Mchungaji Amy Groeschel.

Kuwa Ujasiri Wewe
5 Siku
Mpango huu wa kusoma Biblia wa siku 5 na Yareli Tilan ni mwaliko wa upole wa kugundua tena jinsi unavyopendwa na kuthaminiwa sana machoni pa Mungu. Haijalishi tumetembea na Bwana kwa muda gani, ni rahisi kupoteza mtazamo wa thamani yetu na kuruhusu shaka za kibinafsi ziangukie. Lakini Mungu anatuita watoto Wake wapendwa — na ukweli huo unabadilisha kila kitu. Unapotumia muda katika Maandiko, kutafakari, na kutumia yale unayosoma, moyo wako uwe na uchangamfu, utambulisho wako katika Kristo uimarishwe, na ujasiri wako upya. Ingia katika kila siku kwa uhakika kwamba wewe ni Wewe wa Kujiamini!

Tabia
SIku 6
Mabadiliko si rahisi, lakini si kwamba hayawezekani. Kuanza tabia chache rahisi itabadilisha jinsi unajiona leo na kukugeuza uwe mtu ambaye ungependa kuwa kesho. Mpango huu wa Biblia wa Life.Church unatazama Maandiko ili kutengeneza tabia za kila siku ambazo zitadumu.

Hatua Sita Ya Uongozi Bora Zaidi
Siku 7
U tayari kukua kama kiongozi? Craig Groeschel anafafanua hatua sita ya kibiblia yeyote anaweza kuchukua ili kuwa kiongozi bora zaidi. Gundua nidhamu ya kuanza, ujasiri wa kuacha, mtu wa kumwezesha, mfumo wa kuumba, uhusiano wa kuanzilisha, na hatari ambayo unahitaji kuchukua.

Kukombolewa kwa ndoto
Siku 7
Tunafanyaje wakati ndoto zetu zinapoonekana kuwa haziwezi kutimia? Ukiwa umeshinda matusi na hofu, pamoja na kuvunjika moyo baada ya ndoa kuvunjika, ninakabiliwa na swali mara kwa mara. Ikiwa unapitia uharibifu wa tukio au hasara, au kuchanganyikiwa baada ya kusubiri jambo kwa muda mrefu, ndoto ya Mungu kwa maisha yako bado iko hai! Rafiki ni wakati wa kuwa na ndoto tena.

Yesu Ananipenda
Siku 7
Ikiwa mtu angekuuliza, "Ninahitaji kuamini ipi ili niwe Mkristo?" ungemjibu vipi? Kwa kutumia maneno ya wimbo upendwao, "Yesu anipenda, kweli ninajua, kwani Biblia inasema”, mhubiri aliyekuwa mwanahabari anakusaidia kuelewa unachoamini na sababu. Mwandishi maarufu John S. Dickerson anafafanua imani za kimsingi za Kikristo kwa uwazi na uaminifu na kuashiria mbona imani hizi ni muhimu.

Ishi kwa Nguvu na Ujasiri!
Siku 8
Hauko peke yako. Uwe na siku 1 au miaka 30 katika imani yako ya Kikristo, ukweli huu unasimama thabiti kwa changamoto zote za maisha. Jifunze jinsi ya kukaribisha msaada wa Mungu kwa ufanisi katika mpango huu. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo Kwa Ukuaji na Kusudi” na David J. Swandt

Ibada juu ya Vita vya Akilini
Siku 14
Hii ibada itakusaidia kwa himizo za tumaini la kushinda hasira, machafuko, hukumu, hofu, shaka ... chochote kile. Ufahamu huu utakusaidia kujua njama ya adui ya kukuchanganya na kukudanganya, kukabiliana na mwelekeo wa mawazo ulioharibika, kupata ushindi katika kubadilisha mawazo yako, kupata nguvu, kutiwa moyo na, muhimu zaidi, ushindi juu ya kila vita akilini mwako. Una nguvu ya kupigana ... hata ikiwa ni siku moja kwa wakati!

Mpango Bora wa Kusoma
Siku 28
unajisihisi umezidiwa, kutoridhika, na kukwama maishani? Je unatamani maisha yako ya kila siku yaboreke? Neno la Mungu ni mwongozo kwa siku njema. Katika mpango huu wa siku 28, utagundua njia kutoka kuishi tu maisha mema, hadi kuishi maisha mema ambayo Mungu amekutazamia.