Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mit 3:5

Kugeuka kutoka kwenye mambo ya hisia
Siku 3
Wakati maisha yako hayako katika mpangilio na neno la Mungu ni dhahiri kabisa utapata matokeo ya kuumiza. Wakati hisia zako zonapokuwa hazina mpangilio na zinaanza kupanga maisha yako, unaweza kujikuta umejifungia katika gereza lako mwenyewe ambalo inaweza kuwa vigumu kutoroka. Unahitaji kutafuta uwiano sahihi na ujifunze kumwamini Mungu. Acha Tony Evans akuoneshe njia ya uhuru wa hisia.

Kugeuka Kutoka Katika Masuala Ya Mihemko
Siku 3
Wakati ambapo maisha yako yanatoka katika upatanisho wa neno la Mungu, hakika ni kwamba, utakabiliwa na hali ngumu yenye matokeo yaletayo uchungu. Mihemko yako inapokosa kudhibitiwa nayo ikaanza kuamua ustawi wako, utajikuta umejifungia katika gereza la kujitengenezea ambalo linaweza kuwa vigumu kwako kutoroka. Wahitaji usawaziko, na kujifunza jinsi ya kumtumaini Mungu. Mruhusu Tony Evans akuonyeshe njia ya uhuru wa kimihemko.

Kushinda Kujiamini na Wasiwasi
4 Siku
Mchezaji virukaji wa Uingereza Cindy Sember anashiriki(anaelesea) jinsi alivyoshinda hali ya kutojiamini na wasiwasi katika mashindano. Cindy huwasaidia wanariadha kugeuza mtazamo wao kutoka kwa woga hadi imani, wakitumaini ahadi za Mungu za nguvu. Mpango huu unatoa njia rahisi, za vitendo za kuchukua nafasi ya wasiwasi na uaminifu. Inakusaidia kupata amani na ujasiri katika michezo na maisha. Ni sehemu ya mfululizo wa mashindano ya kutumia kabla, wakati na baada ya kushindana.

Je, nafsi yako
Siku 5
Yuda Smith huwasaidia wasomaji kuchunguza na kuimarisha nafsi zao kama wanavyokua karibu na Mungu.

MUNGU + MALENGO: Jinsi Ya Kuweka Malengo Kama Mkristo
Siku 5
Ni vyema kuweka malengo kama Mkristo. Unajuaje kama lengo lako ni kutoka kwa Mungu au kwako mwenyewe?. Na malengo ya kikristo yanaonekanaje? Katika siku 5 za mpango huu wa kusoma, utajifunza katika neno na kupata ufasaha na muelekeo juu ya kupanga mipango inayosukumwa na neema!

Kukombolewa kwa ndoto
Siku 7
Tunafanyaje wakati ndoto zetu zinapoonekana kuwa haziwezi kutimia? Ukiwa umeshinda matusi na hofu, pamoja na kuvunjika moyo baada ya ndoa kuvunjika, ninakabiliwa na swali mara kwa mara. Ikiwa unapitia uharibifu wa tukio au hasara, au kuchanganyikiwa baada ya kusubiri jambo kwa muda mrefu, ndoto ya Mungu kwa maisha yako bado iko hai! Rafiki ni wakati wa kuwa na ndoto tena.

Yesu Ananipenda
Siku 7
Ikiwa mtu angekuuliza, "Ninahitaji kuamini ipi ili niwe Mkristo?" ungemjibu vipi? Kwa kutumia maneno ya wimbo upendwao, "Yesu anipenda, kweli ninajua, kwani Biblia inasema”, mhubiri aliyekuwa mwanahabari anakusaidia kuelewa unachoamini na sababu. Mwandishi maarufu John S. Dickerson anafafanua imani za kimsingi za Kikristo kwa uwazi na uaminifu na kuashiria mbona imani hizi ni muhimu.

Ibada juu ya Vita vya Akilini
Siku 14
Hii ibada itakusaidia kwa himizo za tumaini la kushinda hasira, machafuko, hukumu, hofu, shaka ... chochote kile. Ufahamu huu utakusaidia kujua njama ya adui ya kukuchanganya na kukudanganya, kukabiliana na mwelekeo wa mawazo ulioharibika, kupata ushindi katika kubadilisha mawazo yako, kupata nguvu, kutiwa moyo na, muhimu zaidi, ushindi juu ya kila vita akilini mwako. Una nguvu ya kupigana ... hata ikiwa ni siku moja kwa wakati!

Mpango Bora wa Kusoma
Siku 28
unajisihisi umezidiwa, kutoridhika, na kukwama maishani? Je unatamani maisha yako ya kila siku yaboreke? Neno la Mungu ni mwongozo kwa siku njema. Katika mpango huu wa siku 28, utagundua njia kutoka kuishi tu maisha mema, hadi kuishi maisha mema ambayo Mungu amekutazamia.