Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Flp 2:10

Kupata Uhuru kutokana na Kufadhaika
Siku 5
Kufadhaika huwa, lakini hakufai kuyaendesha maisha yako. Kumpitia Kristo, tunaweza kuibadilisha, kuiona upya na kuitafsiri upya. Kama unapata changamoto na kufadhaika, angalia mpango huu wa Bibilia wa siku 5 ili ujifunze kupata uhuru na amani.

Pasaka Na Mfalme
5 Siku
Mpango huu wa kusoma Biblia wa siku 5 kwa Pasaka unakualika kusherehekea Yesu Kristo, Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana. Wafalme wa kibinadamu hupokea taji na matukio makubwa, lakini hakuna anayemzidi Yesu. Utawala Wake wa milele unatuletea amani, tumaini, na wokovu. Zaidi ya miaka 2,000 iliyopita, alivaa taji la miiba na kisha akafufuka kwa nguvu, akibadilisha kila kitu. Pasaka hii, furahisha moyo wako na ushindi Wake dhidi ya kifo na umsabahi kama Mfalme wako wa milele!

Nenda Tenda Sema Toa: Uhuru wa Kujisalimisha kwa Yesu
Siku 7
Kujisalimisha kwa Yesu ni tukio kubwa maishani. Lakini uamuzi huu unamaanisha nini na tutauishi vipi kila siku? Uamuzi ni wa mambo makubwa ya maisha pekee, ama wacha Mungu kupita kiasi? Woga, makosa yaliyopita, na kutoelewa vinaweza kutuzuia. "Nenda Tenda Sema Toa" ni ahadi/sala ambayo inafunua jinsi utakavyochukua hatua zinazofuata katika safari yako ya kiroho. Pata uhuru unaotokana na kumfuata Yesu.

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022
Siku 30
Soma Biblia Kila Siku Juni/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Juni pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wafilipi na Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure