Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mt 1:18

Kaa Ndani ya Yesu - Ibada ya Majilio ya Siku 4
Siku 4
Krismasi inakaribia! Pamoja nayo inakuja Majilio – kipindi cha kujiandaa na kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu. Lakini je, ukweli huo unapotea kwa sababu ya ratiba nyingi za msimu wa sikukuu, kununua zawadi bora, au kuandaa mikusanyiko ya familia? Katika harakati za msimu wa Krismasi, pata njia mpya za kuhusiana na Neno la Mungu, ambazo zitakuvuta karibu zaidi naye. Amsha nafsi yako kupitia mpango huu wa kusoma wa siku 4 kutoka kwa Abide Bible Journals za Thomas Nelson.

Hadithi ya Krismasi: Siku 5 kuhusu Kuzaliwa kwa Yesu
Siku 5
Krismasi hii, rejelea hadithi ya kuzaliwa kwa Yesu katika Injili Takatifu ya Mathayo na Luka. Unaposoma, video fupi yaeleza kila upande wa hadithi kwa kila siku ya mpango huu.

Imani Juu Ya Hofu
26 Siku
Majira ya Maajilio yanatualika kuandaa mioyo yetu kwa ajili ya kuja kwa Yesu, si kwa sherehe tu bali pia kwa tafakari. Katika simulizi ya Krismasi, hofu ni dhima inayojirudia: hekaluni, kwenye ndoto, milimani na hata kwenye nyumba za utulivu. Lakini kila mara, Mungu hatoi hukumu bali anatupa hakikisho: 'Usiogope.' Katika tafakari fupi fupi za mfululizo huu, tunachunguza jinsi kuchagua imani badala ya hofu kunavyotusaidia kumkaribisha Yesu kwa kina zaidi katika maisha yetu.

SOMA BIBLIA KILA SIKU 01/20
Siku 31
Soma Biblia Kila Siku 01/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Kutoka, Zaburi na Isaya. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Anza mwaka wa 2020 kwa kujifunza Neno la Mungu kupitia mpango huu.
