Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Isa 40:30

Ishi kwa Nguvu na Ujasiri!
Siku 8
Hauko peke yako. Uwe na siku 1 au miaka 30 katika imani yako ya Kikristo, ukweli huu unasimama thabiti kwa changamoto zote za maisha. Jifunze jinsi ya kukaribisha msaada wa Mungu kwa ufanisi katika mpango huu. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo Kwa Ukuaji na Kusudi” na David J. Swandt

Upendo wa Kweli ni nini?
Siku 12
Kila mtu anataka kujua upendo ni kitu gani. Lakini watu wachache huangalia ni nini Biblia inasema kuhusu upendo. Upendo ni mada moja muhimu ya Maandiko na pia wema muhimu zaidi katika maisha ya Kikristo. Mpango huu kutoka Huduma za Thistlebend unashughulikia maana ya kibiblia ya upendo na jinsi ya kuboresha kumpenda Mungu na kuwapenda wengine.

Mwaka Mpya, Rehema Mpya
SIku 15
Kwa siku 15 zifuatazo, Paul David Tripp atakukumbusha kuhusu neema ya Mungu kwako—ukweli ambao daima si wa kale. Wakati ambapo “urekebishaji wa tabia” na semi za kukutia moyo hazitoshi kukufanya uwe mtu mpya, jifunze kutumainia wema wa Mungu, kutegemea neema yake, na kuishi kwa ajili ya utukufu wake kila siku.