Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na 1 Pet 5:7

Kukumbuka yale yote Mungu ametenda.
Siku 5
Ni tabia yetu ya asili kutazamia siku zijazo lakini tusisahau kamwe siku zilizopita. Mpango huu umechapishwa kwa ajili yako katika siku 5 zijazo kukukumbusha yote ambayo Mungu amekutendea katika kukutengeneza kuwa ulivyo leo Kila siku utapata somo la biblia na ibada fupi iliyoundwa kukusaidia kukumbuka matukio muhimu katika kutembea kwako na Kristo.

Ninakungoja Hapa, Njia ya Majirio ya Tumaini
Siku 7
Majirio ni majira ya matarajio na maandalizi. Ungana na mchungaji na mwandishi Louie Giglo katika safari ya majirio kupata ufahamu ya kuwa kungojea siyo kuharibu hasa unapomngojea Bwana. Shikilia nafasi ya kupata ufunuo na tumaini katika safari hii ya majirio. Katika siku saba zijazo utapata amani na himizo kwa nafsi yako kama vile matarajio kuelekea sherehe!

Usijisumbue kwa Lolote
siku 7
Ingekuwaje kama kungekuwa na njia bora ya kupigana na hofu isiyoisha inayokufanya kukosa usingizi? Pumziko halisi lipo--yawekana karibu zaidi ya unavyofikiria. Badilisha hofu na amani kupitia siku hizi 7 za mpango wa Biblia kutoka Life.Church, ikiambatana na mfululizo wa ujumbe wa Mchungaji Craig Groeschel Usijisumbue kwa Lolote.

Mazungumzo na Mungu
Siku 12
Kuongea na Mungu ni furaha ya kuzama katika maisha ya maombi, ukisisitiza njia sahihi za kusikia sauti ya Mungu. Mungu anatutaka tufurahie mazungumzo endelevu pamoja naye katika maisha yetu yote - mazungumzo yanayoleta tofauti katika mwelekeo, mahusiano, na kusudi. Mpango huu umejaa uwazi, hadithi binafsi kuhusu kuufikia moyo wa Mungu. Anatupenda!

Kuwa Karibu Na Mungu Kila Siku
Siku 14
Katika mpango huu wa ibada ya Siku 14 Joyce husaidia wasomaji kufikia maisha ya ujasiri zaidi, yenye furaha kwa kukua karibu katika uhusiano wao na Mungu.

Soma Biblia Kila Siku 11/2020
Siku 30
Soma Biblia Kila Siku 11/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

Jolt ya Furaha
Siku 31
Biblia inatuambia kwamba "Katika uwepo wake kuna furaha tele" na kuwa "furaha ya Bwana ni nguvu yetu". Furaha sio hisia tu bali ni tunda la Roho na mojawapo ya silaha bora katika gala letu la kupigana na kuvunjika moyo, huzuni na kushindwa. Tumia siku 31 ukijifunza ni nini Biblia inasema kuhusu Furaha na kujiimarisha kuwa Mkristo mwenye Furaha bila wasi wasi.