1
Yakobo 3:17
Neno
NEN
Lakini hekima inayotoka mbinguni kwanza ni safi, kisha inapenda amani, tena ni ya upole, iliyo tayari kusikiliza wengine kwa unyenyekevu, iliyojaa huruma na matunda mema, isiyopendelea mtu, tena isiyokuwa na unafiki.
Compară
Explorează Yakobo 3:17
2
Yakobo 3:13
Ni nani aliye na hekima na ufahamu miongoni mwenu? Basi na aioneshe hiyo kwa maisha yake mema na kwa matendo yake yaliyotendwa kwa unyenyekevu utokanao na hekima.
Explorează Yakobo 3:13
3
Yakobo 3:18
Mavuno ya haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani.
Explorează Yakobo 3:18
4
Yakobo 3:16
Kwa maana panapokuwa na wivu na ubinafsi, ndipo penye machafuko na uovu wa kila namna.
Explorează Yakobo 3:16
5
Yakobo 3:9-10
Kwa ulimi tunamhimidi Bwana na Baba yetu, na kwa huo twawalaani watu walioumbwa kwa mfano wa Mungu. Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haistahili kuwa hivyo.
Explorează Yakobo 3:9-10
6
Yakobo 3:6
Ulimi pia ni moto, ndio ulimwengu wa uovu kati ya viungo vya mwili. Ulimi huutia mwili wote wa mtu unajisi na kuuwasha moto mfumo mzima wa maisha yake, nao wenyewe huchomwa moto wa Jehanamu.
Explorează Yakobo 3:6
7
Yakobo 3:8
lakini hakuna mtu awezaye kuufuga ulimi. Ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti.
Explorează Yakobo 3:8
8
Yakobo 3:1
Ndugu zangu, msiwe walimu wengi, kwa maana mnafahamu kwamba sisi tufundishao tutahukumiwa vikali zaidi.
Explorează Yakobo 3:1