1
Marko MT. 6:31
New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921
SWZZB1921
Akawaambia, Njoni ninyi peke yenu kwa faragha, mahali pasipo watu, mkapumzike kidogo. Kwa sababu walikuwako watu wengi, wakija, wakienda, hatta haikuwapo nafasi ya kula.
Харьцуулах
Marko MT. 6:31 г судлах
2
Marko MT. 6:4
Yesu akawaambia, Nabii hakosi heshima, illa katika inchi yake, na kwa jamaa zake, na katika nyumba yake.
Marko MT. 6:4 г судлах
3
Marko MT. 6:34
Yesu aliposhuka chomboni, akaona makutano mengi, akawahurumia, kwa sababu walikuwa kana kondoo wasio mchunga; akaanza kuwafundisha mengi.
Marko MT. 6:34 г судлах
4
Marko MT. 6:5-6
Wala hakuweza kufanya mwujiza wo wote huko, isipokuwa aliweka mikono yake juu ya wagonjwa wachache, akawaponya. Akastaajahu kwa sababu ya kutokuamini kwao. Akazungukazunguka katika vile vijiji, akifundisha.
Marko MT. 6:5-6 г судлах
5
Marko MT. 6:41-43
Akaitwaa ile mikate mitano na zile samaki mbili, akatazama mbinguni, akavibariki, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi wake awaandikie: na zile samaki mbili akawagawia wote. Wakala wote wakashiba. Wakaokota vipande vilivyomegwa vya kuweza kujaza vikapu thenashara: navyo vipande vya samaki.
Marko MT. 6:41-43 г судлах
Нүүр хуудас
Библи
Тѳлѳвлѳгѳѳнүүд
Бичлэгүүд