Лого на YouVersion
Икона за пребарување

Hekima Ya KirohoПримерок

Hekima Ya Kiroho

1 ДЕН ОД 3

Hekima ya kiroho inatokana na kuwa na mizizi katika maarifa yetu ya Mungu (Waefeso 1:17).

Ombi la Paulo kwa ajili ya Wakristo wa Efeso lilikuwa kwamba Mungu awape roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua Yeye. Kisha Paulo alieleza ujuzi huu mkuu zaidi wa Mungu kama kujua tumaini la mwito wake, utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu, na ukuu usio na kipimo wa uweza wake kwetu sisi tunaoamini (Waefeso 1:18 – 20).

Hekima ya kiroho inaweza fafanuliwa kama, kufanya maamuzi yanayotegemea maoni na mtazamo wake Mungu. Tunapoendelea kumjua Mungu kwa undani zaidi, tunapata mtazamo wake kuhusu hali zetu na kupata hekima Yake ya kiroho kwa maamuzi yetu.

Je, unaweza kuelezea vipi barabara ambayo umekuwa ukisafiria hivi majuzi katika safari yako ya maisha? Je, unakabiliwa na maamuzi magumu na misukosuko na hali iliyojipinda pinda? Tulia sasa umuombe Mungu hekima yake kwa hali na maamuzi yanayokukabili.

Свето Писмо