Injili Ulimwenguni - Sehemu 2Pavyzdys

Nikodemo
Basi palikuwa na mtu mmoja Farisayo, jina lake Nikodemo, mmoja wa Baraza la Wayahudi lililotawala.
Huyu alimjia Yesu usiku akamwambia," “Rabi, tunajua kuwa wewe ni mwalimu uliyetumwa na Mungu, kwa maana hakuna mtu awezaye kufanya miujiza hii uifanyayo wewe, kama Mungu hayuko pamoja naye. Yesu akamjibu, “Amin, amin nakuambia, mtu hawezi kuuona Ufalme wa Mungu asipozaliwa mara ya pili.” Nikodemo akauliza,“Awezaje mtu kuzaliwa wakati akiwa mzee? Hakika hawezi kuingia mara ya pili kwenye tumbo la mama yake ili azaliwe!”
Yesu akamwambia, “Amin, amin nakuambia, hakuna mtu ye yote anayeweza kuingia katika Ufalme wa Mungu isipokuwa amezaliwa kwa maji na kwa Roho.
"Mwili huzaa mwili, lakini Roho huzaa roho. Kwa hiyo usishangae ninapokuambia huna budi ‘kuzaliwa mara ya pili.’
Upepo huvuma po pote upendapo. Mvumo wake unausikia lakini huwezi ukafahamu utokako wala uendako. Ndivyo ilivyo kwa kila mtu aliyezaliwa na Roho.”
Nikodemo akamwuliza, “Mambo haya yanawezekanaje?” Yesu akamwambia, “Wewe ni mwalimu mashuhuri wa Waisraeli, nawe huelewi mambo haya?
Amin, amin ninakuambia, sisi tunazungumza lile tunalolijua na tunashuhudia lile tuliloliona. Lakini ninyi watu hamkubali ushuhuda wetu. "Nimewaambia mambo ya duniani, nanyi hamkuniamini, mtaniaminije basi nitakapowaambia mambo ya mbinguni? Hakuna mtu ye yote aliyekwenda mbinguni isipokuwa yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani, Mwana wa Adamu.
Kama vile Mose alivyomwinua yule nyoka kule jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa juu. "Ili kila mtu amwaminiye awe na uzima wa milele.
“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Kwa maana Mungu hakumtuma Mwanawe kuuhukumu ulimwengu, bali kwa yeye ulimwengu upate kuokolewa.
Šventasis Raštas
Apie šį planą

Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadithi ambacho kinafuata masimulizi ya Agano Jipya yanayopatikana katika vitabu vya Injili vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana.
More
Susiję planai

Išrinkta – atskleidžiant moterį Kristuje

Paveskite savo rūpesčius

Sėklos: Kokios ir kodėl

Koks mano tikslas? Mokomės mylėti Dievą ir kitus žmones

Himnas: Malonė tavo istorijoje

Kelkis ir nušvisk

Džiaugsmas kelionėje: Atrandant viltį išmėginimų sūkuryje

Meilė ir santuoka, autorius Billy Graham

Mylėkite ir nenustokite mylėję
