1
Matendo 20:35
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
TKU
Daima niliwaonesha kwamba mnapaswa kufanya kazi nilivyofanya na kuwasaidia wadhaifu. Niliwafundisha kukumbuka maneno ya Bwana Yesu aliyosema, ‘Ni baraka kuu kutoa kuliko kupokea.’”
Compara
Explorar Matendo 20:35
2
Matendo 20:24
Siujali uhai wangu mwenyewe. Jambo la muhimu zaidi ni mimi kuimaliza kazi yangu. Ninataka niimalize huduma ambayo Bwana Yesu alinipa niifanye, nayo ni kuwahubiri watu Habari Njema kuhusu neema ya Mungu.
Explorar Matendo 20:24
3
Matendo 20:28
Jilindeni ninyi wenyewe pamoja na watu wote mliopewa na Mungu. Naye Roho Mtakatifu amewapa ninyi kazi ya kuwachunga kondoo hawa. Ni lazima muwe wachungaji wa kanisa la Mungu, watu ambao Mungu aliwanunua kwa damu ya Mwanaye wa pekee.
Explorar Matendo 20:28
4
Matendo 20:32
Sasa ninawaweka katika uangalizi wa Mungu. Ninategemea ujumbe wa neema yake kuwaimarisha ninyi. Ujumbe huo unaweza kuwapa ninyi baraka ambazo Mungu huwapa watakatifu wake wote.
Explorar Matendo 20:32