Zaburi 67

67
Wimbo wa shukrani
1Kwa mukubwa wa waimbaji. Kwa vyombo vyenye nyuzi. Zaburi. Wimbo.
2Utuonee huruma, ee Mungu, utubariki,
utuelekezee uso wako kwa wema,
3dunia yote ipate kutambua njia yako,
mataifa yote yajue nguvu yako ya kuokoa.
4Watu wakusifu, ee Mungu,
watu wote wakusifu!
5Mataifa yote yafurahi na kuimba kwa furaha;
maana unawahukumu watu kwa usawa,
na kuyaongoza mataifa katika dunia.
6Watu wakusifu, ee Mungu,
watu wote wakusifu!
7Inchi imetoa mazao yake;
Mungu, Mungu wetu, ametubariki.
8Mungu aendelee kutubariki.
Watu wote katika dunia wamwabudu.

Цяпер абрана:

Zaburi 67: SWC02

Пазнака

Капіяваць

Параўнаць

Падзяліцца

None

Хочаце, каб вашыя адзнакі былі захаваны на ўсіх вашых прыладах? Зарэгіструйцеся або ўвайдзіце