Soma Biblia Kila Siku 04/2025预览

Sadaka ya hatia ilihusiana na makosa kama vile kutumia vitu vilivyowekwa wakfu isivyotakiwa, au kupoteza vitu vya mtu mwingine, kwa mfano kwa kumdanganya katika jambo la amana. Sadaka hii huambatana na fidia ya asilimia ishirini ya thamani kamili. Yule mnyama aliyekufa badala ya mwenye dhambi hutakiwa kuwa kondoo mume mkamilifu. Yesu alipokufa alitoa sadaka kamili ya hatia, si asilimia ishirini tu, maana alitoanafsi yake iwe fidia ya wengi(Mk 10:45), ili sisi tuwe hai kwa njia ya mauti yake.
读经计划介绍

Soma Biblia Kila Siku 04/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Aprili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Walawi, Luka na 2 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu
More