Soma Biblia Kila Siku 04/2025预览

Soma Biblia Kila Siku 04/2025

30天中的第8天

Haruni na wanawe ndio waliopewa wajibu wa kusogeza sadaka za watu kwenye madhabahu. Mazingira, vyombo vilivyotumika, na kuhani alivyofanya, mambo yote yalitakiwa kutekelezwa kwa uangalifu mkubwa kwa jinsi Mungu alivyoagiza. Kwa mfano, makuhani waliruhusiwa kula nyama ya sadaka, isipokuwa kama damu ya mnyama ililetwa ndani ya hema ya kukutania, basi wasile nyama yake. Hali hii inatukumbusha jinsi Yesu alivyokuwa mwangalifu sana kutimiza masharti yote alipofanya upatanisho kwa ajili dhambi zetu.

读经计划介绍

Soma Biblia Kila Siku 04/2025

Soma Biblia Kila Siku 04/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Aprili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Walawi, Luka na 2 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu

More