Soma Biblia Kila Siku 03/2025预览

Soma Biblia Kila Siku 03/2025

31天中的第9天

Hamkumbuki(m.18)?Wanafunzi walikuwa wameona miujiza mikubwa wakati Yesu alipowashibisha maelfu ya watu. Sasa wako chomboni wakiwa na mkatemmoja tu. Wakasumbukia jambo hili, tena wakabishana. Ni kana kwamba wamesahau yote yaliyopita. Ni wazito kuamini uwezo wa Yesu. Na Yesu akawalaumu. Hata sisi Wakristo wa siku hizi ni wepesi kusahau. Bila shaka kila mmoja wetu angeweza kusimulia jinsi Mungu alivyowahi kumsaidia. Na Yesu hajabadilika. Bado ni yeye yule. Tukumbushane, na tuitikie kama ilivyoandikwa katika Zab 103:2:Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, Wala usizisahau fadhili zake zote.

读经计划介绍

Soma Biblia Kila Siku 03/2025

Soma Biblia Kila Siku 03/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko, 1 Nyakati na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu

More