Soma Biblia Kila Siku 03/2025预览

Soma Biblia Kila Siku 03/2025

31天中的第10天

Aliye heri ni mtu anayefahamu mahali pa kukimbilia wakati wa mtafaruku. Daudi alifahamu pa kugeukia. Ni kwa Mungu. Kwa hiyo anaanza kwa ombi la kupata msaada. Mara mbili anamwomba Mungu, “Uniponye”; na pia anasihii,“Uniokoe”(m.1-2). Anajiona yuko kwenye hatari toka wale anaowaeleza kama “watu wa damu”(m. 12). Mapokeo ya zamani husema hao ni watu waliotumwa na Sauli ili wamwue Daudi. Duniani tunaishi katika misukosuko mingi ya maisha. Tumwombe Mungu. Ndiye awezaye kutuokoa. Kumbuka ilivyoandikwa katika Zab 55:22: “Umtwike BWANA mzigo wako naye atakutegemeza, hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele.

读经计划介绍

Soma Biblia Kila Siku 03/2025

Soma Biblia Kila Siku 03/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko, 1 Nyakati na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu

More