Soma Biblia Kila Siku Juni/2022预览

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022

30天中的第7天

Unyenyekevu wa Kristo ni mfano mzuri kwetu. Aliacha utukufu wa kimbingu. Alijishusha kuwa mtumishi, hata akaaibishwa katika msalaba. Akawa mtumishi asiyethamanika. Lakini Mungu alimzawadia jina kubwa kuliko majina yote. Na sasa kila kiumbe kitamsujudia. Hivyo ndivyo itupasavyo Wakristo kuishi: Mungu huwalipa wanyenyekevu baraka nyingi duniani. Hatimaye atawaita mbinguni, atawapa kurithi pamoja na Kristo. Ukitamani hayo, ishi kwa unyenyekevu kama Kristo.

读经计划介绍

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Juni pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wafilipi na Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More