Soma Biblia Kila Siku Mei 2021预览

Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni na kuiamini Injili (Mk 1:15). Maneno haya ya Yesu tungeweza kuweka kama kichwa juu ya utumishi wa mitume. Wakatoka, wakahubiri kwamba watu watubu (m.12). Ndivyo walivyowaambia watu, na ndivyo sisi Wakristo wa leo tunavyotakiwa kuwaambia watu. Na ili watu watambue kwamba ufalme wa Mungu umekaribia, Yesu akafanya miujiza kwa mikono yao. Hata leo hufanya hivyo. Zingatia kwamba Yesu akawatuma wawili wawili (m.7). Utaratibu huu wa Yesu ni jambo la kutendea kazi kwa viongozi wa kanisa la leo!