Soma Biblia Kila Siku Mei 2021预览

Kupaa kwa Yesu ni tendo la Yesu kuondoka kimwili hapa duniani na kwenda mbinguni kwa Mungu. Kuna faida pia kwetu, kwani Yesu aliahidi kwenda kutuandalia makao ambapo wote wanaomwamini wataishi naye baadaye. Pia alitoa ahadi ya kutuletea Roho Mtakatifu ili atuongoze, atutie nguvu na kutufariji katika huduma yetu (Mdo 1:8). Mpaka leo Yesu yupo kati yetu kwa njia ya Roho Mtakatifu, na baraka alizotoa kwa wanafunzi wake zipo kwa wote wanaoliitia jina lake. Mwamini Yesu ili atakapokuja akukute upo tayari, na ukaurithi uzima wa milele.