Soma Biblia Kila Siku 06/2020预览

Soma Biblia Kila Siku 06/2020

30天中的第28天

Katika huduma ya Yesu tunasikia mara chache kwamba ugonjwa wa mtu ulisababishwa na pepo. Jana tulisoma kwamba alimponya mtu mwenye ugonjwa wa kawaida wala hakuwa na pepo. Lakini leo anamponya mtu ambaye anaonekana kuwa na ugonjwa wa kawaida, hata hivyo udhaifu wa mwili wake ulisababishwa na pepo. Hata Tanzania haya yanatokea. Lakini tusifikiri kwamba magonjwa yote husababishwa na pepo. Bali ni mara chache. Tusimtie hofu mtu kwa kudai kwamba ana pepo mchafu ikiwa ana ugonjwa wa kawaida tu!

读经计划介绍

Soma Biblia Kila Siku 06/2020

Soma Biblia Kila Siku 06/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Yohana, Ayubu na Mathayo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More