Soma Biblia Kila Siku 8预览

Musa anaendelea kukumbusha na kukazia maneno yaliyotolewa na Bwana hapo mlimani Sinai miaka 40 iliyopita alipofanya agano na Waisraeli. Kizazi kipya cha taifa la Israeli sasa kimepata kulisikia Neno la Agano. Watakapokwisha ingia Kaanani, ni muhimu wajisimamishie mawe makubwa na kuyapigia lipu (m.2-3: Iwe, siku mtakayovuka Yordani kwenda nchi akupayo Bwana, Mungu wako, ujisimamishie mawe makubwa, ukayatalize matalizo, uyaandike maneno yote ya torati hii juu yake, utakapokwisha kuvuka; ili upate kuingia nchi akupayo Bwana, Mungu wako, nchi imiminikayo maziwa na asali, kama alivyokuahidi Bwana, Mungu wa baba zako). Ndipo waandike juu yake maneno yote ya agano waliyoyasikia sasa. Kazi ya mawe haya ni kuwakumbusha Waisraeli na kuwa ushahidi juu ya uaminifu wa Mungu na mapenzi yake. Kisha wamtolee Bwana sadaka, na wote wale pamoja machoni pake wakilifurahia agano.