Soma Biblia Kila Siku 8预览

Maonyo na mafundisho juu ya njia ya hekima toka kwa wazazi wamchao Mungu yapaswa kuzingatiwa na watoto, kwa kuwa hekima ndiyo inayomkuza mtu (m.8:Umtukuze, naye atakukuza; Atakupatia heshima, ukimkumbatia). Eneo muhimu katika mafundisho ya wazazi ni kuelekeza upendo, utii na heshima kwa Mungu. Itikio la Mungu kwa watakaozingatia ya wazazi, ni kuwatuza tuzo bora! Lakini pia kama ilivyoandikwa katika Kutoka 20:12, maisha marefu ni zawadi kwa wanaowaheshimu wazazi: Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako. Watoto wanapowasikiliza wazazi, wanampenda Mungu aliyetoa amri hii.